Welcome to the Lugha Zetu Forums, a space dedicated to connecting people through African languages and cultures. Our forums bring together languages from different countries, creating opportunities for discussion, learning, and collaboration across diverse linguistic communities. If you do not see your language represented, we would love to hear from you. Please let us know so we can continue to grow and include more languages in our community. Join the conversation, share your knowledge, and be part of a space that celebrates lugha zetu—our languages.
Je, kuna lahaja ngapi za Kiswahili?
Kuna lahaja nyingi za Kiswahili kutoka mwambao wa Afrika Mashariki (baina ya kusini mwa Somalia na kaskazini mwa Msumbiji) hadi barani kufikia sehemu za Afrika ya Kati. Baadhi ya lahaja hizi ni: Kimvita (Mombasa), Kiamu na Kipate (Lamu), Kimrima na Kimtangata (sehemu za pwani ya Tanzania), Kiunguja mjini (Unguja), Kipemba na Kihadimu (Pemba), Kimakunduchi (Unguja), Kitumbatu (Kisiwa cha Tumbatu), Chimwini na Kibajuni (Pwani ya Somalia), Makwe na Mwani (Mpaka wa Tanzania na Msumbiji), Kingwane (Kusini Mashariki ya Kongo), na Kisheng (Sehemu za Nairobi).
Wazungumzaji wa lahaja hizi kwa kiasi kikubwa wanaelewana. Lakini, baadhi ya wakati, kuna uwezekano wa kutoelewana kutokana na tofauti ya matamshi, istilahi, na sarufi.
Kwa niaba ya Ustadh Abdilatif Abdalla:
Hilo neno *mbwa* (kwa silabi moja) liko pia katika Kiswahili cha kale, na latumika mpaka hivi leo katika baadhi ya lahaja za Kiswahili za Pwani ya Kenya katika lugha ya kawaida na katika lugha ya kishairi. Nalo ni muunganiko wa maneno mawili: *ni* na *wa.*; na latumika katika hali ya umoja na wingi pia. Kwa mfano, _Mtoto huyu/Watoto hawa *mbwa* nani?_ (= Mtoto huyu/ Watoto hawa ni wa nani?). Kama ni wa rafiki yangu nitajibu: *Mbwa* rafiki yangu (= Ni wa rafiki yangu). Na kama ni wangu, nitajibu: *Mbwangu* (= Ni wangu). Neno hili laweza kutumika pia katika ngeli ya M/MI na ngeli ya U, lakini katika hali ya umoja tu: _Mti *mbwangu*_ (= Mti ni wangu); __Udongo_ *_mbwa_* _kufinyangia vyungu_ (= Udongo ni wa...); _Ufunguo wake *mbwa* shaba_(= ...ni wa shaba).
*Abdilatif Abdalla*
Hamburg, Ujerumani
20 Novemba, 2026.
